11.8 C
New York

Simeone: Barcelona walituzidi kila kona

Published:

MADRID, Hispania

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amekiri kuwa wapinzani wao, Barcelona, walikuwa bora zaidi ndani ya uwanja katika mchezo waliofungwa mabao 2-1.

Simeone ameweka wazi kuwa vijana wake hawakuwa kwenye ubora wa kushindana na Barcelona, hivyo wanapaswa kuamka katika mechi zijazo.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu [La Liga], Barcelona walizoa pointi zote tatu kwa mabao ya Fermin Lopez aliyefunga mawili, huku Atletico wakijifuta makocha kwa bao la Giuliano Simeone.

Akizungumza baada ya dakika 90 za mechi hiyo, Simeone amesema: “Waliweza kutumia nafasi walizotengeneza, walikuwa hatari zaidi kwenye kushambulia kuliko sisi.”

Kwa matokeo hayo, Barcelona wanabaki kileleni mwa msimamo wa La Liga, wakati Atletico Madrid wako nafasi ya tatu nyuma ya Madrid.

Related articles

Recent articles