ANKARA, Uturuki
MWAKA 2026 unatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa na joto kali zaidi kuwahi kutokea, kwa mujibu wa Wanasayansi katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza [BBC].
Wanasayansi wameeleza kuwa kuongezeka kwa joto kunatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, sambamba na El Nino.
Berkeley Earth, moja ya taasisi za tafiti za utabiri wa hali ya hewa za Marekani, imeeleza kuwa kuna uwezekano wa asilimia 95 kwamba joto la mwaka 2026 ni kali zaidi kuwahi kutokea.
Mwaka 2024 utakumbukwa kwa kuwa na joto kali zaidi lakini wanasayansi wanaamini 2026 itaivunja rekodi hiyo.
Wiki iliyopita, Shirika la Hali ya Hewa la Umoja wa Ulaya lilitaja mwezi uliopita [Oktoba] kuwa ndiyo mwezi uliokuwa na joto kali zaidi katika historia ya dunia.


