14.3 C
New York

Wasomali wafariki wakizamia kuingia Ugiriki

Published:

ATHENS, Ugiriki

WAHAMIAJI takribani 13, wengi wao wakiwa ni raia wa Somalia, wamefariki baada ya boti iliyokuwa ikiingia Ugiriki kuzama katika Pwani ya Crete.

Kwa mujibu wa waokoaji, watu 18 waliokolewa na wote walikuwa wakitokea Somalia kuingia Ugiriki. Wanne kati yao wanaendelea na matibabu.

Mmoja ya waokoaji ambaye hata hivyo hakutaka jina lake kuwekwa hadharani, amesema waliokolewa walikutwa kwenye hali mbaya kutokana na kupigwa na baridi kali.

Licha ya kutokufahamika haraka kwa chanzo cha ajali hiyo, mamlaka zimedai kuwa huenda ilitokana na upepo mkali.

Ajali za majini zimeendelea kushika kasi katika safari za wahamiaji wanaoingia Ulaya wakitokea Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini.

Takwimu zinaeleza kuwa wahamiaji Zaidi ya 22,000 wameingia Ugiriki, na hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu pekee.

Related articles

Recent articles