WASHINGTON DC, Marekani
MELANIA Trump ambaye ni mke wa Rais Donald Trump, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Ukraine na Urusi na kuzitaka pande mbili hizo kumaliza vita.
Katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu ya Marekani, Melania amesema vita hivyo vimeathiri kwa kiasi kikubwa wananachi wasio na hatia kutoka pande zote mbili.
Ukraine katika mazungumzo hayo iliwakilishwa na mjumbe wa haki za binadamu, Dmytro Lubinets, pia akiwepo Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Davyd Arakhamia.
Baada ya mazungumzo yake na wawakilishi, Melania aliwakabidhi barua maalumu za kuwapelekea marais wa nchi zao.
Kwa upande wake, wachambuzi wa siasa wamempongeza Melania kwa jitihada yake kubwa iliyofanikisha siku sita za bila mapigano katika eneo la Oleshky .


