20.3 C
New York

Deschamps akataa kazi Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

LICHA ya kwamba hana kazi kwa sasa, kocha wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, ameipiga chini ofa ya kuinoa Manchester United.

Kwa mujibu wa kile kilichoripotiwa na Gazeti la Dailly Mirror, mabosi wa Man United wamewasiliana na Deschamps wakijaribu kumshawishi avae viatu vya Michael Carrick anayeweza kutimuliwa wikiendi hii.

Taarifa ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na Man United, Carrick anaweza kufungashiwa virago endapo timu hiyo itafungwa Jumapili hii katika mchezo wao dhidi ya Aston Villa.

Hata hivyo, ripoti zinaeleza kuwa Deschamps amewaambia Man United kwamba havutiwi na mpango wa kuwa kocha mpya Old Trafford.

Deschamps, kiungo wa zamani wa Ufransa, amejijengea heshima kubwa katika ulimwengu wa soka, hasa baada ya kunyakua Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha wa kikosi hicho.

Related articles

Recent articles