20.3 C
New York

Papa aanza ziara baada ya afya kuimarika

Published:

ROMA, Italia

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Leo XIV, anaanza ziara yake ndefu kuelekea Kusini mwa Amerika zikiwa ni wiki tatu tu tangu alipofanyiwa upasuaji wa saratani ya mapafu.

Katika ziara hiyo, mbali na maeneo mengine, Papa Leo ataitembelea Peru, nchi ambayo aliwahi kuhudumu kama padri kwa miaka mingi.

Kwa mujibu wa mamlaka za Vatican, hali ya afya ya sasa ya kiongozi wake huyo haihitaji uangalizi kwani alifanyiwa operesheni na kupona kabisa.

Papa Leo [71], alifanyiwa upasuaji mwezi uliopita baada ya vipimo vya madakrari kubaini uvimbe kwenye mapafu yake ya upande wa kulia.

Baadaye, vipimo hivyo vilibaini kuwa saratani yake haikuwa imesambaa kwenye maeneo mengine ya mwili, hivyo upasuaji tu ungetosha kumuweka kumuondoshea tatizo hilo.

Mbali na Peru, ziara hiyo inatarajiwa kumpelekea Papa Leo katika nchi zingine kubwa za Amerika Kusini, Uruguay na Argentina.

Related articles

Recent articles