ASUNCION, Paraguay
RAIS wa Paraguay, Santiago Pena, ametangaza kujiuzulu baada ya mkwamo wa kisiasa uliosabishwa na anguko la moja ya benki nchini humo.
Pena amejiweka kando baada ya wanasiasa wa upinzani kumjia juu kwa kitendo cha Benki ya Ueno kufikilisika na kusitisha shughuli zake.
Kilichomponza zaidi ni kwamba Pena alikuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni iliyokuwa ikimiliki benki hiyo.
“Nataka kuwaomba radhi watu wote kama nilishindwa kwa namna yoyote ile,” amesema katika ujumbe wake kwa njia ya video huko mitandaoni.
Kabla ya kutangaza uamuzi huo, tayari yalikuwapo maandamano nje ya ofisi yake yakishinikiza aondoke madarakani.


