19.1 C
New York

Kipa Liverpool kurudi Brazil

Published:

RIO, Brazil

MLINDA mlango wa Liverpool, Alisson Becker, huenda akaondoka klabuni hapo na kurejea kwao kujiunga na klabu ya Flamengo.

Becker [34], ameingia kwenye miezi 12 ya mwisho wa mkataba wake na vigogo hao wa Anfield, hivyo atakuwa mchezaji huru Juni, 2027.

Ni kwa maana hiyo, kipa huyo ataondoka bure ifikapo mwishoni mwa msimu huu endapo Liverpool itashindwa kumshawishi kuongeza mkataba mpya.

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za michezo wa Sport Witness, Becker amevutiwa na mpango wa kujiunga na Flamengo ya mjini Rio de Janeiro.

Hata hivyo, kwa sasa Flamengo inakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi inayoweza kuzuia kumudu mshahara mnono wa kipa huyo.

Related articles

Recent articles