LIBREVILLE, Gabon
MTAMBO wa kuchimba mafuta baharini umezama nchini Gabon, huku watu 110 waliokuwa ndani yake wakiokolewa na wengine watano wakiendelea kutafutwa.
Katika taarifa yake, kampuni ya BW Energy imesema watu wote 110 waliokuwa ndani ya mtambo huo wakati wa ajali waliokolewa, huku juhudi za kuwatafuta waliopotea zikiendelea.
Rais wa Gabon, Brice Clotaire Oligui Nguema, amesema operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji inaendelea, huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Kwa mujibu wa kampuni inayomiliki mtambo huo, ajali ilitokea wakati wa operesheni ngumu ya kuunyanyua mtambo huo. Nguzo zake za kuuegemeza zinaripotiwa kuzama kwenye sakafu ya bahari, hali iliyosababisha mtambo kupoteza uthabiti na kuzama kwa haraka.
Mtambo huo ulikuwa umepangwa kutumika kuchimba visima vinne vya mafuta kwa niaba ya kampuni ya BW Energy ya Norway.


