22.2 C
New York

Ripoti yaanika maumivu haya sekta ya afya

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

TAASISI ya Uwajibikaji wa Umma [WAJIBU] kupitia Ripoti yake ya Mwaka 2024-25, imebaini uhaba wa asilimia 54.7 ya wahudumu kwenye sekta ya afya nchini.

Sambamba na hilo, Ripoti imeeleza kuwa licha ya Serikali kugharamia zaidi ya Shilingi bilioni 5.17, vifaa vilivyonunuliwa havijaanza kutumika katika halimashahuri 28 nchini.

Miongoni mwa sababu za kutokutumika kwake ni uhaba wa wataalamu, kutokukamilika kwa ujenzi wa majengo, umeme usio wa uhakika, na ubovu au kukosekana kabisa kwa miundombinu ya maji.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa Septemba 25, 2026, imeeleza kuwa kwa sasa sekta hiyo ilihitaji wafanyakazi 379,766 lakini ilipata 172,122, hivyo kuwapo kwa uhaba wa wengine 207,644.

Aidha, katika baadhi ya vituo vya afya, zimekuwapo mashine za kisasa lakini bado hazijaanza kutoa huduma, kwa mujibu wa Ripoti hiyo ya WAJIBU.

Pia, baadhi ya vituo vya afya kati ya 30 vilivyokaguliwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG], baadhi yamuuguzi au mkunga mmoja alilazimika kuhudumia wanawake wajawazito takribani 10.

Related articles

Recent articles