9.3 C
New York

Hispania mabingwa Kombe la Dunia U-20

Published:

MADRID, Hispania

TIMU ya soka ya Taifa ya Hispania ya U-20 kwa upande wa wanawake imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa ushindi wa penalti dhidi ya Korea ya Kaskazini.

Timu hizo zilivaana jana Septemba 27, 2026, katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Miejski LKS Lodz nchini Poland.

Dakika 90 na zile 30 za nyongeza zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na ndipo Hispania ilipoibuka na ushindi wa penalty 4-3.

Fainali hiyo ilitanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu, ambapo U-20 ya Colombia iliifunga Italia kwa staili hiyo hiyo ya mikwaju ya penalti [4-3] baada ya sare ya bao 1-1.

Aidha, michuano hiyo imemalizika kwa wachezaji watatu wa Hispania kuondoka na tuzo. Laia Lopez ameibuka na tuzo ya Kipa Bora, Rosalia Dominguez ni Kinda Bora na Pau Comendador amekuwa Mfungaji Bora.

Related articles

Recent articles