19.1 C
New York

Natamba nae kumrudisha Kelvin Bosco kwa kishindo

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, mwimbaji wa muziki wa injili nchini, Kelvin Bosco, anatarajia kurejea kwenye muziki kwa kishindo kupitia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la “Natamba Nae”, unaotarajiwa kutoka Oktoba 1.

Tangu alipotangaza ujio wa wimbo huo, Kelvin amesema amekuwa akipokea shauku kubwa kutoka kwa mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii, huku wengi wakisubiri kwa hamu kusikia kazi yake mpya.

Akizungumza na www.gazetini.co.tz Kelvin Bosco alisema “Natamba Nae” ni mwendelezo wa kazi zake za kumsifu Mungu, huku ujumbe wake ukilenga kuonyesha umuhimu wa kutambua na kusherehekea uwepo wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.

“Wimbo utatoka Oktoba 1 katika mitandao yote ya muziki. Naamini nitawashtua mashabiki zangu ambao wamenisubiri kwa muda mrefu sana. Naomba wakae mkao wa kuhudumiwa na wimbo huu,” amesema Kelvin Bosco.

Mwimbaji huyo amewataka mashabiki wake kuendelea kusubiri kwa hamu ujio wa kazi hiyo, ambayo anatarajia itawafikia watu mbalimbali kupitia majukwaa ya muziki mtandaoni.

Related articles

Recent articles