LONDON, Uingereza
NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, amegomea tena ofa ya kusaini mkataba mpya klabuni hapo, na hiyo inaendeleza tetesi za kiungo huyo kutimka Old Trafford ifikapo mwishoni mwa msiu huu.
Mkataba wake na ‘Mashetani Wekundu’ utafikia ukomo Juni, 2027, ingawa klabu hiyo kipo kipengele kinachoipa klabu hiyo nafasi ya kumuongeza miezi 12.
Hata hivyo, kwa kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa hadi sasa, uwezekano wa nyota huyo kutimka ni mkubwa. Je, ni wapi ataibukia mchezaji huyo?
SPORTING LISBON
Klabu hiyo ya mjini Lisbon, Ureno, ndiyo iliyompa jina kubwa baada ya kufunga mabao 63 katika mechi 137 tangu aliposajiliwa akitokea Sampdoria. Hadi anajiunga na Man United mwaka 2020, Bruno ndiye aliyekuwa nahodha wa timu hiyo.
Katika mahojiano yake ya mwaka 2025, Bruno alionesha nia ya kurudi Sporting akisema: “Nimewahi kufikiria kuhusu kurudi Ureno,” alisema nyota huyo.
JUVENTUS
Amewahi kucheza soka nchini Italia akiwa na Novara, Udinese na Sampdoria iliyomuuza kwa Sporting mwaka 2017. “Nina uhusiano mkubwa sana na nchi hiyo. Binti yangu alizaliwa pale na amekuwa akisema anataka kujifunza Kiitaliano,” aliwahi kusema Bruno.
Kwa Italia, Juventus inaweza kuwa klabu sahihi kwake kwani nayo inahaha kusaka ubigwa wa kwanza wa Ligi Kuu [Serie A] tangu ilipouchukua mwaka 2020.
ATLETICO MADRID
Wakati Fulani, Atletico Madrid iliwahi kuhusishwa na Bruno na huu unaweza kuwa wakati sahihi zaidi kwa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya soka nchini Hispania [La Liga].
Bruno anaweza kuwa msaada mkubwa kwa kocha Diego Simeone katika kushindana na Real Madrid na Barcelona kwenye La Liga na mashindano mengine ya ndani.
AL HILAL
Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia imeonesha mara kadhaa tamaa yake ya kumsajili staa huyo. Ilitenga kitita cha Pauni milioi 100 mwaka 2025 lakini Manchester United walikataa.
Wakati ambao mabosi wa klabu hiyo walimtangazia Bruno mshahara wa kufuru wa Pauni 700,000 [takribani Sh bil. 3 za Tanzania] kwa wiki. “Rais wa Al Hilal alinipigia simu na kuniuliza …” alisema Bruno.


