29 C
New York

Apandikiziwa figo ya nguruwe, yamsogeza siku 271

Published:

LOS ANGELES, Marekani

FIGO ya nguruwe iliyopandikizwa kwa mgonjwa imemsaidia kuishi siku 271, kwa mujibu wa madaktari nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mgonjwa huyo aliyefahamika kwa jina la Tim Andrews, figo hiyo ya nguruwe ilimpa tumaini la kuishi walau kwa siku chache hizo wakati akisubiri zoezi la kusafishwa damu.

Ni baada ya siku hizo, figo ya nguruwe aliyopandikizwa ilishindwa kufanya kazi, lakini tayari ilishapatikana ya binadamu kwa ajili ya kuwekewa.

Aidha, timu ya madaktari wa Hospitali ya Mass General Brigham wameeleza kuwa hiyo inathibitisha kuwa figo ya binadamu inaweza kumsogeza mgonjwa wakati akisubiri ipatikane ya kupandikiziwa.

Mafanikio hayo yamekuwa wakati huu madaktari na wanasayansi wakiendelea kutafiti namna figo za viumbe wengine zinavyoweza kumsaidia binadamu.

Kwa Marekani, uhaba wa figo za binadamu ni mkubwa, ambapo kuna uhitaji wa watu takribani 100,000. Uingereza uhaba ni figo zaidi ya 7,000.

Related articles

Recent articles