30.8 C
New York

EPL siyo mchezo kwa matumizi soko la usajili

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU za Ligi Kuu ya England [EPL] zilitumia kiasi cha Pauni bilioni 3.46 katika soko la usajili wa majira haya ya kiangazi lililofungwa hivi karibuni [Septemba 1, 2026].

Kati ya fedha hizo, Pauni milioni 475 zilitumika siku ya mwisho ya usajili, ikilinganishwa na Pauni 391 za mwaka jana.

Aidha, kiasi cha Pauni bilioni 3.46 cha mwaka huu ni kikubwa zaidi kuwahi kutumika katika historia ya klabu za EPL kwenye soko la usajili.

Manchester City ndiyo klabu iliyoongoza kwa kutumia fedha nyingi, ambapo ilimwaga jumla ya Pauni milioni 458, ikifuatiwa na Chelsea [Pauni Mil. 349], na Tottenham [Pauni Mil. 303].

Chini ya kocha mpya, Enzo Maresca, Man City ilimsajili mchezaji wa bei mbaya zaidi, Enzo Fernandez, ambaye aliigharimu Pauni milioni 125 kumng’oa Chelsea.

Wakati huo huo, Enzo anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya EPL kuuzwa kwa ada ya zaidi ya Pauni milioni 100.

Liverpool, kwa upande wao, walivunja rekodi yao ya usajili kwa kumchukua winga kutoka PSG, Bradley Barcola, aliyegharimu kiasi cha Pauni milioni 123.

Kwa upande mwingine, Tottenham nao walivunja rekodi yao ya usajili walipokubali kuipa Newcastle United kiasi cha Pauni milioni 100 kumchukua Sandro Tonali.

Related articles

Recent articles