24 C
New York

Klabu zilizovunja rekodi usajili wa kiangazi 2026

Published:

LONDON, Uingereza

MANCHESTER City imevunja rekodi yake ya usajili majira haya ya kiangazi kwa kumchukua kiungo Enzo Fernandez kwa ada ya Pauni milioni 125. Nyota huyo ametokea Chelsea.

Kwa upande wao, Chelsea nao walivunja rekodi yao ya usajili walipomnasa Morgan Rogers kutoka Aston Villa, ambapo uhamisho wake uligharimu Pauni milioni

Wakati huo huo, Aston Villa wao walimfanya Nicolas Jackson kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo baada ya kuipa Chelsea kitita cha Pauni milioni 65.

Katika hatua nyingine, Tottenham imevunja rekodi yao ya usajili kwa kuipa Newcastle United kitita cha Pauni milioni 100 ili kuinasa saini ya kiungo raia wa Italia, Sandro Tonali.

Coventry City, timu mpya kwenye Ligi, ilivunja rekodi yake ya usajili kwa kumchukua Caleb Yirenkyi kutoka Nordsjaelland, dili hilo likiigharimu kitita cha Pauni milioni 26.

Leeds United nao wamevunja rekodi yao ya usajili. Ni baada ya kumchukua kipa kutoka Manchester City, James Trafford, ambaye ameigharimu Pauni milioni 40.

Aidha, Hull City nao hawajabaki nyuma. Beki wa kati, Nobel Mendy, amekuwa mchezaji wa bei mbaya zaidi, Pauni milioni 22, kuwahi kusajiliwa klabuni hapo.

Ipswich Town, kwa upande wao, nao walivunja rekodi ya usajili baada ya kumnasa Emersonn kutoka Toulouse kwa ada ya Pauni milioni 26.6.

Brighton walitumia Pauni milioni 50 kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kumchukua Luka Vuskovic kutoka Tottenham, wakati kiungo Mamadou Sangare na beki El Hadji Malick Diouf wamekuwa wachezaji ghali zaidi kwa Hull City, kila mmoja akigharimu Pauni milioni 40.

Nottingham Forest nayo imevunja rekodi yake ya usajili baada ya kutumia Pauni milioni 50 kumsajili Liam Delap kutoka Chelsea. Awali, rekodi ilikuwa ikishikiliwa na Omari Hutchinson ambaye Forest ilimsajili kwa Pauni milioni 12.5 akitokea Ipswich.

Related articles

Recent articles