19.8 C
New York

Rais Trump atangaza hatua mpya Venezuela

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS Donald Trump amesema Marekani imefikia makubaliano ya kudhibiti mapipa zaidi ya bilioni 65 ya mafuta ghafi kutoka Venezuela.

Kwa mujibu wa Rais Trump, ametamba kuwa mapipa hayo yataongeza mara mbili akiba ya mafuta nchini Marekani.

Wakati huo huo, kupitia mitandao ya kijamii, amejinasibu kuwa hatua hiyo inakwenda kupunguza bei ya gesi kwa raia wa Marekani.

Kwa upande wake, Rais wa Mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez, ameiita hatua hiyo kuwa ni muhimu kwa uchumi wa nchi yake.

Marekani imekuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuchumi nchini Venezuela tangu ilipoivamia na kumng’oa madarakani Rais Nicolas Maduro.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Marekani, Marco Rubio, ameeleza kuwa makubaliano ya sasa yana faida kwa pande zote.

Related articles

Recent articles