25.2 C
New York

Serikali, M23 na safari ya kutafuta amani DRC

Published:

KINSHASA, DRC

WAWAKILISHI wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Kundi la waasi la M23 wamekutana mjini Geneva, Uswis, na kukubaliana kuweka silaha chini na kurejesha amani nchini humo.

Hii ni hatua nyingine, ukiacha ile ya mwaka 2025 iliyosimamiwa na Marekani, ambapo pande mbili hizo zilikutana mjini Doha, Qatar, na kujadili namna ya kumaliza vita.

Safari hii, makubaliano ni kwamba kitaundwa chombo maalumu chini ya MONUSCO (Kikosi cha Jeshi la Kulinda Usalam la Umoja wa Mataifa (UN) kuhakikisha pande mbili hizo zinaacha kabisa kushambuliana.

Marekani, Qatar, Umoja wa Afrika (AU) na Uswis zimeeleza kuunga mkono mchakato huo wa kuhakikisha amani inarejea, hasa maeneo ya Mashariki mwa Taifa la DRC.

Tangu mwaka 2022, vita kati ya wanejeshi wa Serikali na waasi wa M23 vimesababisha mamia kuua na wengine kukimbia makazi yao.

M23 wanaendelea kutawala sehemu kubwa ya North Kivu na South Kivu, majimbo makubwa mawili ya Mashariki mwa DRC yenye utajiri mkubwa wa madini.

Kwa upande mwingine, wachambuzi wa siasa, akiwamo Alex Vines, Mkurugenzi wa Programu za Afrika kutoka Baraza la Umoja wa Ulaya, Kitengo cha Mahusiano ya Kimataifa, bado wanahofia utajiri huo wa madini unaweza kuzigombanisha tena pande mbili hizo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Uanaharakati wa Amani (CPRA), Cliffton Chifuwe, anasema changamoto iliyopo ni kwamba M23 si kikundi pekee cha uasi huko Mashariki mwa DRC. “Vikundi vipo vingi,” amesema.

Aidha, Chifuwe ameongeza kuwa pia kuna hali ya kutokuaminiana kati ya DRC na Rwanda inayotajwa kuwapa msaada wa kijeshi na kifedha M23.

Related articles

Recent articles