26.5 C
New York

Yanga yaipigisha kwata JKT, yaitandika ‘4G’

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

USHINDI wa tatu mfululizo. Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa leo Agosti 24, 2026.

Yanga ikiwa nyumbani katika Uwanja wa KMC, imefikisha pointi tisa baada ya kushinda mechi mbili za awali msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo wa leo uliochezwa kwenye Uwanja KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, Yanga ilipata mabao yake matatu ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Mshambuliaji raia wa Zambia, Albert Kangwanda, alifunga bao la kwanza dakika ya 29, likiwa ni la pili kwake msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Mabao mengine ya Wanajangwani hao yalifungwa na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (Dk. 34), Chadrack Boka (Dk. 38) na Peter Shalulile (Dk. 63).

Matokeo hayo yameiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi ikiwa na pointi tisa, ikilingana na Simba inayoshika nafasi ya pili.

Kwa upande mwingine, kituo kinachofuata kwa ‘Timu ya Wananchi’ ni mechi dhidi ya Pamba Jiji itakayochezwa Agosti 28, 2026.

Related articles

Recent articles