27.1 C
New York

Yanga mwendo mdundo, yaikaanga Coastal Union

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MABINGWA watetezi msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wameshinda mechi yao ya pili kwa kuifunga Coastal Union mabao 4-1.

Matokeo hayo ni baada ya Yanga kuanza Ligi kwa ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa mkoani Lindi siku chache zilizopita.

Katika mchezo huo wa leo Agosti 20, 2026, uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, Yanga ilimaliza kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko ikiwa tayari inaongoza kwa mabao 2-0.

Nyota mpya raia wa Zambia, Albert Kangwanda, alikuwa wa kwanza kuipatia Yanga bao katika dakika ya 39 na hilo linakuwa bao lake la pili katika mechi mbili za msimu huu wa Ligi.

Yanga iliporejea uwanjani, ilipata mabao mengine kupitia kwa Maxi Nzengeli (Dk. 45) na Mudathir Yahya (Dk. 50) na Mohamed Hussein (Dk 93). Coastal walipata bao la kufutia machozi dakika ya 78 lakini halikutosha kuinasua katika kichapo hicho.

Baada ya matokeo ya leo, Yanga imekaa kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi sita, sawa na Simba inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba watakuwa ugenini Agosti 22, 2026 kuivaa Singida Black Stars na Yanga watacheza siku mbili baadaye ikiwa nyumbani dhidi ya JKT Tanzania.

Related articles

Recent articles