23.7 C
New York

Rais Trump na Baraza la Mawaziri la mabilionea

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

VIGOGO wote 57 walioteuliwa na Rais Donald Trump katika awamu yake ya pili madarakani ni matajiri wa kutupwa. Kila mmoja ana utajiri usiopungua Dola milioni 100, kwa mujibu wa Taasisi ya Public Citizen.

Wanasiasa hao wa Chama cha Republican ni pamoja na mabalozi 17 na wengine 40 wanashikilia nyadhifa kubwa ndani ya Serikali Kuu.

Katika Baraza lake la Mawaziri, nane kati ya 23 wanaingia kwenye orodha hiyo ya matajiri wazito, wakiwamo Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Howard Lutnick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Linda McMahon.

Pia, orodha ya mabilionea katika Serikali ya Rais Trump inayo majina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Stephen Feinberg, Katibu Mkuu wa Hazina, Scott Bessent, na Mjumbe Maalumu, Steve Witkoff.

Ni tofauti na uongozi uliopita wa Rais Joe Biden, ambao ulikuwa na mabilionea watano pekee katika ngazi za juu serikalini. Utawala wa Obama ulikuwa na mabilionea watatu pekee.

Aidha, uwepo wa matajiri katika nafasi za juu za juu serikalini umezua maswali juu ya uongozi wa Rais Trump, kwa mujibu wa ripoti ya Public Citizen.

Ifahamike kuwa orodha hiyo haimuhuishi Rais Trump ambaye pia ni bilionea (Dola bilioni 6), pamoja na mshirika wake, Elon Musk, binadamu tajiri zaidi duniani (Dola bilioni 860).

“Inapotokea matajiri wakawa na nafasi za juu serikalini, inazalisha wizi na rushwa na inafikirisha; wako kwa masilahi ya nani?,” anahoji Lisa Gilbert, rais mwenza wa Public Citizen.

Hata hivyo, Rais Trump ana mtazamo tofauti. Anaamini wenye mafanikio makubwa kiuchumi wana uwezo mzuri wa kushauri na hata kufanya maamuzi.

Related articles

Recent articles