LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Andy Burnham, amesema Serikali yake inaiunga mkono Ukraine kwa asilimia 100 na itaendelea kufanya hivyo.
Kauli yake hiyo inakuja baada ya taarifa zinazodai kuwa Ukraine ilitumia ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa Uingereza kuishambulia Urusi.
“Tutakuwa popote pale Ukraine itakapokuwa na uhitaji, na hilo halitobadilika,” amesema Waziri Mkuu huyo.
Hivi karibuni, Urusi iliishitumu Uingereza ikidai imekuwa ikiunga mkono mashambulizi yanayofanywa na Ukraine. “Kwa kadiri (Uingereza) inavyojihusisha, italipia,” amesema.
Akijibu vitisho hivyo, Burnham amesema Uingereza inaisaidia Ukraine ili iweze kujilinda na ubabe wa Urusi.
Kwa siku za hivi karibuni, Ukraine imeendelea kuyashambulia maeneo kadhaa ya Urusi, ukiwamo Mji Mkuu wa Moscow.


