23.7 C
New York

Rooney aitaka United kumsajili staa wa Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Manchester United, Wayne Rooney, ameishauri klabu hiyo kumsajili ‘fasta’ nyota wa Arsenal mwenye umri wa miaka 19, Myles Lewis-Skelly.

Rooney anaamini ujio wa beki huyo wa kushoto utaongeza kitu kwenye kikosi cha kocha Michael Carrick msimu huu wa 2026-27.

“Sidhani kama unaweza kutegemea Luke Shaw atakuwa na kiwango bora msimu mzima,” amesema Rooney.

Kwa mujibu wa Rooney, Lewis-Skelly ni chaguo sahihi endapo Man United itamsajili na uzuri ni kwamba haipatikani kwa fedha nyingi.

“Kama unaweza kumpata mchezaji anayeweza kucheza beki wa kushoto, na pia nafasi ya kiungo wa kati, nafikiri si vibaya kumsajili,” amesema.

Lewis-Skelly alipandishwa timu ya wakubwa ya Arsenal mwaka 2024 akitokea timu ya wakubwa. Mkataba wake utafikia ukomo mwaka 2030.

Related articles

Recent articles