Na mwandishi wetu, Gazetini
KAMA zilivyo zingine, sekta hii nayo itakuwa kichocheo muhimu cha mageuzi ya kiuchumi ifikapo mwaka 2050. Kwanini?
Mahitaji ya huduma za kifedha, bima na uwekezaji yatakua kwa kiasi kikubwa kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa miji.
Huduma bora za kifedha zitaimarisha upatikanaji wa mikopo, kukuza uwekezaji, kuweka akiba, na kuimarisha mbinu za ujasiriamali, na hivyo kurasimisha shughuli za kiuchumi.
Ili kunufaika na huduma hizi, ni muhimu kufanya mabadiliko ya sera, sheria na kanuni mbalimbali.
Kwa upande mwingine, ni muhimu kuwapo kwa maboresho ya miundombinu ya kidijitali na kupunguza gharama za mikopo.
Ifahamike kuwa lengo la Tanzania kuelekea mwaka 2050 ni kuwa na mfumo jumuishi wa fedha, ambao utachangia kukua kwa uchumi.


