27.5 C
New York

Infantino anachota mshahara wa bil. 12/-

Published:

NYON, Uswis

HIVI karibuni, kiongozi huyo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) alikuwa Colombia kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya wa Taifa hilo la Amerika Kusini, Abelardo de la Espriella.

Alipotua katika uwanja wa ndege, Gianni Infantino alipokelewa na rafiki yake, Ramon Jesurun, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la Colombia.

Katika safari yake hiyo, Gianni Infantino aliambatana na Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika ya Kusini (CONMEBOL), Alejandro Dominguez.

Kama ilivyokuwa katika ziara yake nchini Morocco siku chache zilizopita, Infantino alitua Colombia kwa ndege binafsi, msafara wake ukipambwa na magari ya kifahari aina ya Mercedes, huku ukisindikizwa na polisi.

Kama itakumbukwa, hata wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026, alitumia ndege binafsi kusafiri kwenda viwanjani kutazama mechi walau mbili kila siku.

Kwa sehemu kubwa, msafara wake umekuwa na hadhi wanayopewa marais wa nchi nyingi anazotembelea kwa ziara za kikazi, ikiwamo kuangalia maendeleo ya soka.

Aprili, 2026, wakati wa Mkutano Mkuu wa FIFA uliofanyika Canada, mamlaka za nchi hiyo ziligoma Infantino kupewa msafara wa hadhi ya Rais wao.

Pia, wakati wa fainali za Kombe la Dunia za Wanawake mwaka 2023, wenyeji New Zealand nao walikataa kumpa heshima ya hali ya juu kama hiyo.

Kuhusu mshahara, Infantino kwa sasa analipwa mara tatu ya kiasi alichokuwa akipewa wakati anaingia madarakani mwaka 2016.

Miaka 10 iliyopita, alikuwa akilipwa Pauni milioni 1.3 (Sh bil. 4.6 za Tanzania) kwa mwaka lakini mshahara wake umepanda na sasa anavuna kitita cha Pauni milioni 4 (Sh bil. 12.3).

Mtangulizi wake, Sepp Blatter, alikuwa akilipwa Pauni milioni 2.6 katika mwaka wake wa mwisho ndani ya Shirikisho hilo la soka.

Nje ya mshahara huo mnono, Infantino analipwa Pauni 20,500 kwa mwaka kwa ajili ya kujikimu katika gharama za maisha.

Related articles

Recent articles