26 C
New York

Chicharito atua Daraja la Kwanza

Published:

DALAS, Marekani

UNAMKUMBUKA straika wa zamani wa Real Madrid, Manchester United na timu ya soka ya Taifa ya Mexico, Javier Hernandez ‘Chicharito’? Mwamba bado anakipiga.

Akiwa na umri wa miaka 38 kwa sasa, Chicharito amejiunga na Atletico Dallas inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Marekani (USL Championship).

Nyota huyo amesajiliwa na Atletico Dallas na kusaini mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji wa kwanza kutua klabuni hapo majira haya ya kiangazi.

Klabu yake ya mwisho kucheza kabla ya dili hilo ni Chivas ya Mexico, ambayo aliachana nayo Novemba, 2025.

Chicharito aliyewahi pia kupita Bayer Leverkusen na West Ham United, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Mexico akiwa na mabao 52 katika mechi 109.

Related articles

Recent articles