29.1 C
New York

Arsenal, Vinicius Jr dili lao liko hivi

Published:

LONDON, Uingereza

WAKATI huu Real Madrid ikijaribu kumshawishi Vinicius JR kusaini mkataba mpya, Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Huu ni mwaka wa mwisho katika mkataba wa Vinicius Jr, hivyo endapo Madrid hawatomuongeza au kumuuza kipindi hiki, ataondoka bure (akiwa mchezaji huru) mwaka 2027.

Madrid walilipa Pauni milioni 40 tu kumng’oa Flamengo mwaka 2019 lakini sasa thamani yake sokoni imepanda na kufikia Pauni milioni 119.6.

Hata hivyo, Marid itapata chini ya kiasi hicho ikiwa itamuuza kwani tayari amebakiza miezi 12 katika mkataba wake.

Kwa mujibu wa ripoti, Arsenal au klabu nyingine inayomtaka majira haya ya kiangazi inapaswa kuandaa Pauni milioni 90.

Hata hivyo, watapaswa kufumua bajeti yao ya mishahara kwani nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 analipwa Pauni 340,000 kwa wiki pale Madrid.

Katika kikosi chao, mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ni winga raia wa Uingereza, Bukayo Saka, ambaye anachota Pauni 300,000 kwa wiki, akifuatiwa na Kai Havertz (Pauni 280,000). Kwa sasa, Arsenal haionekani kuwa na shida ya pesa kwani ilivuna Pauni milioni 770 msimu uliopita (2025-26) baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Related articles

Recent articles