Na mwandishi wetu, Gazetini
KWA mwaka 2025, idadi ya wahamiaji nchini Marekani ilipungua kutoka milioni 2.7 hadi milioni 1.3, idadi ndogo zaidi katika historia ya nchi hiyo kubwa kiuchumi.
Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Sensa la Marekani, takribani nusu ya wahamiaji hao milioni 1.3 walikimbilia katika majimbo matano.
Jimbo la Florida liliongoza kwa kuchukua wahamiaji wapya wengi (178,674, sawa na asilimia 14.2), likifuatiwa kwa karibu na Texas (167,475, sawa na asilimia 13.3).
Nafasi ya tatu ilishikwa na California kwa wahamiaji 109,300 (8.7%), huku New York ikiwa ya nne kwa wahamiaji 95,600 (7.6%).
Majimbo mengine yaliyopokea wahamiaji wengi kwa mwaka 2025 ni New Jersey (53,100), North Carolina (46,900), Washington (46,200), Illinois (44,800), na Georgia (42,600).
Ni kama ilivyokuwa kwa Virginia (40,400), Massachusetts (40,200), Michigan (30,700), Ohio (28,500), Arizona (28200), Pennsylvania (26,900), Maryland (20,500), na Tennessee (18,000).


