NIAMEY, Niger
WANASHERIA wa Rais wa zamani wa Niger, Mohamed Bazoum, wameomba kiongozi huyo aachiwe huru, ikiwa ni miaka mitatu tangu aliposhikiliwa na jeshi.
Bazoum mwenye umri wa miaka 66, alichaguliwa mwaka 2021, kabla ya mapinduzi ya kijeshi kumng’oa madarakani mwaka 2023.
Tangu hapo, Rais huyo na mkewe, Hadiza, wamekuwa chini ya jeshi mjini Niamey. Wanasheria wake wamedai kuwa anashikiliwa kinyume cha sheria.
“Hawajawahi kupelekwa mahakamani na wala hawajawahi kuambiwa mashitaka yanayowakabili,” amesema Mwanasheria Reed Brody.
Wakati Bazoum anakamatwa, kiongozi wa jeshi, Jenerali Abdourahamane Tiani, aliahidi kumfungulia mashitaka, jambo ambalo ni miaka mitatu sasa halijatokea.


