NEW DELHI, India
MAANDAMANO makubwa ya vijana wa Gen-Z nchini India yamemlazimisha Waziri wa Elimu, Dharmendra Pradhan, kuachia ngazi.
Hatua ya vijana, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, kuingia barabarani ilikuja baada ya Wizara ya Elimu kufuta mitihani kwa kigezo cha maswali kuvuja.
Katika ujumbe wao kwa Serikali, vijana walitaka Waziri wa Elimu, Pradhan, kujiuzulu, kabla ya kuibua ishu zingine, ikiwamo ukosefu wa ajira.
Akizungumzia kujiuzulu kwake, Waziri huyo amesema: “Kwa kuzingatia kinachoendelea nchini, pia kunusuru majanga zaidi, nimemwandikia Waziri Mkuu barua ya kujiuzulu.”
Baada ya taarifa za Waziri kujiuzulu, kiongozi wa Chama cha Vijana cha CJP, Abhijeet Dipke, alisema: “Kazi imekwisha.”


