21 C
New York

Sikia hii ya Arteta na makocha EPL

Published:

LONDON, Uingereza

KATI ya makocha 20 wa Ligi Kuu ya England (EPL) kwa msimu ujao wa 2026-27, ni watatu tu walioziongoza timu zao kwa zaidi ya miaka mitatu. Mikel Arteta wa Arsenal ndiye aliyedumu kwa muda mrefu, akiwa ameiongoza timu hiyo tangu Desemba 22, 2019.

Anayefuta ni Eddie Howe, ambaye amekuwa kwenye benchi la ufundi la Newcastle United tangu November 8, 2021. Katika nafasi ya tatu ni kocha wa Aston Villa, Unai Emery, akiwa ameliongoza benchi la ufundi la timu hiyo tangu November 1, 2022.

Nafasi ya nne ni Daniel Farke, ambaye mabosi wa Leeds United walimpa ajira Julai 4, 2023, na waliobaki ni Regis Le Bris (Sunderland, 2024), Fabian Hurzeler (Brighton, 2024), Frank Lampard (Coventry, 2024), na David Moyes (Everton, 2025).

Wengine ni Sergej Jakirovic (Hull City, 2025), Keith Andrews (Brentford, 2025), Michael Carrick (Man United, 2026), na Roberto De Zerbi (Tottenham, 2026).

Pia, kuna Marco Rose (B’mouth, 2026), Andoni Iraola (Liverpool, 2026), Pierre Sage (Palace, 2026), na Gary O’Neil (Ipswich, 2026), Enzo Maresca (Man City, 2026), Xabi Alonso (Chelsea, 2026), Oliver Glasner (Nottingham, 2026), na Alvaro Arebola (Fulham, 2026).

Related articles

Recent articles