BOSTON, Marekani
RUDI GARCIA wa Ubelgiji ni miongoni mwa makocha waliojikuta kwenye wakati mgumu katika fainali zilizopita za Kombe la Dunia.
Itakumbukwa kuwa Garcia aliondoka kwenye benchi baada ya timu hiyo kuishia hatua ya robo fainali, wakiondoshwa na Hispania.
Pape Thiaw wa Senegal naye alifukuzwa baada ya safari ya timu hiyo kuishia hatua ya 16 Bora, kama ilivyokuwa kwa Julian Nagelsmann (Ujerumani) na Ronald Koeman (Uholanzi).
Vilevile, makocha waliopoteza vibarua kwa timu zao kuishia hatua hiyo ni Zlatko Dalic (Croatia), Roberto Martinez (Ureno) na Sebastian Beccacece (Ecuador).
Aidha, wengine waliyaacha mabenchi ya ufundi baada ya timu zao kuishia hatua ya makundi. Makocha hao ni Marcelo Bielsa (Uruguay) na Hong Myung-bo (Korea Kusini).
Wakati huo huo, orodha hiyo ina majina ya makocha Miroslav Koubek (Czech), Steve Clarke (Scotland) na Sabri Lamouchi (Tunisia).


