28 C
New York

Ugonjwa wa Ebola bado kizungumkuti DRC

Published:

KINSHASA, DRC

WATU zaidi ya 1,000 wameshapoteza maisha ndani ya miezi miwili ya ugonjwa wa Ebola nchini DRC, idadi kubwa zaidi, ikilinganishwa na mlipuko wa mwaka 2014 na 2016.

Katika ripoti ya Wizara ya Afya ya DRC, visa 2,536 na vifo 1,033 vimejitokeza tangu maambukizi ya Ebola y’all kuripotiwa Mei 15, 2026.

Ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 2014 na 2016, ambapo vifo 1,000 vilifika baada ya miezi nane ya ugonjwa. Safari hii, ni ndani ya miezi miwili tu.

Tofauti na Ebola zilizopita, safari hii ugonjwa huo unasababishwa na virusi aina ya Bundibugyo, ambavyo hadi sasa wataalamu wa afya hawajafanikiwa kuvipatia chanzo wala tiba yake.

Aidha, mlipuko wa Ebola uko katika majimbo matano pekee ya mikoa ya Mashariki mwa DRC, pamoja na nchi jirani ya Uganda, huku visa vichache vikiripotiwa Marekani na Ulaya.

Ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 2014 na 2016, ambapo ugonjwa huo ulisambaa zaidi barani Afrika katika mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Hata hivyo, safari hii wastani wa kupoteza maisha baada ya kupata maambukizi ni asilimia 40, ikilinganishwa na asilimia 60 kwa mwaka 2014 na 2016.

Related articles

Recent articles