24.9 C
New York

Meneja wa muziki ataka kujiua

Published:

LAGOS, Nigeria

MENEJA maarufu wa wasanii wa muziki nchini Nigeria, Ubi Franklin, amefichua kuwa aliwahi kukaribia kujiua kwa kujirusha darajani jijini Lagos.

Franklin ameanika hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akieleza mashabiki wake juu ya maisha aliyopitia.

Kwa mujibu wake, alikaribia kujitoa uhai baada ya kuachwa na mkewe, Lilian Esoro, bila sababu, licha ya utajiri wake mkubwa.

Kupitia Instagram, amesema alikwenda hadi kwenye daraja kwa lengo la kujirusha ili aondoke duniani, kabla ya binamu wake, Omini Stitches, kuwahi na kumuokoa.

“Nilikuwa kwenye kipindi cha msongo wa mawazo. Nakumbuka wakati fulani niliendesha gari hadi Daraja la Mainland ili nikajiue,” amesema.

Related articles

Recent articles