28.7 C
New York

‘Kufuru’ ya fedha Kombe la Dunia 2026

Published:

MIAMI, Marekani

KWA kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka huu (2026), timu ya soka ya Taifa ya Hispania imelamba kitita cha Dola za Marekani milioni 50 (takribani Sh bil. 132 za Tanzania).

Argentina ya Lionel Messi, licha ya kukosa taji kwa kufungwa bao 1-0, imechota Dola milioni 33 (Zaidi ya Sh bil. 87 za Tanzania).

Aidha, England iliyoshika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ufaransa mabao 6-4 imejiondokea na Dola milioni 29 (takribani Sh bil. 77 za Tanzania).

Wakati huo huo, mabingwa wa fainali za mwaka 2018, Ufaransa, hawakuondoka patupu, na badala yake wamejipatia Dola milioni 27 (Sh bil. 71.2 za Tanzania).

Timu zilizoshika nafasi ya tano hadi ya nane zimeweka mfukoni kiasi cha Dola milioni 19 (Sh bil. 50.1 za Tanzania) kila moja, ambazo ni Norway, Ubelgiji, Morocco na Uswis.

Katika nafasi ya tisa hadi ya 16, kila moja imejinyakulia kitita cha Dola milioni 15 (takribani Sh bil. 40 za Tanzania). Timu hizo ni Mexico, Colombia, Brazil, Marekani, Ureno, Canada, Misri na Paraguay.

Pia, zilizoshika nafasi ya 17 hadi ya 32 zimeingiza Dola milioni 11. Timu hizo ni Uholanzi, Ujerumani, Ivory Coast, Croatia, Japan, Australia, DRC, Ghana, Ecuador, Afrika Kusini, Sweden, Bosnia, Algeria, Senegal, na Cape Verde.

Zilizoshika nafasi ya 33 hadi ya mwisho (48) nazo zimebeba Dola milioni 9 kila moja, ambazo ni Iran, Korea Kusini, Uturuki, na Scotland.

Zingine ni Uruguay, Saudi Arabia, Czech, New Zealand, Qatar, Curaçao, Panama, Jordan, Haiti, Uzbekistan, Tunisia, na Iraq.

Ikumbukwe, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo Juni 11, 2026, kila timu ilishapatiwa Dola milioni 1.5 kwa ajili ya maandalizi tu.

Hivyo, fainali za mwaka huu zimeshuhudia ongezeko kubwa la fedha za bingwa, ikilinganishwa na zile zilizopita za mwaka 2018 na 2022.

Bingwa wa mwaka 2018, Ufaransa, alizoa Dola milioni 38. Kwa mwaka 2022, Argentina ilibeba ‘ndoo’ na kujinyakulia Dola milioni 42.

Related articles

Recent articles