25.2 C
New York

Messi anacheka kwa dharau, atuma ujumbe

Published:

MIAMI, Marekani 

NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi, amezipuuza taarifa zinazodai kuwa wanabebwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Messi (39), amesema hakuna ukweli wowote juu ya ripoti hizo, akisistiza kuwa watu wanapaswa kuendelea kufurahia burudani ya soka kutoka kwao.

Kauli hiyo imekuja baada ya Argentina kutinga fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa wa mwaka 1966, England.

Katika mchezo huo wa jana Julai 15, 2026, Messi alitoa asisti katika mabao yote mawili, wafungaji wakiwa ni Enzo Fernandez na Lautaro Martinez.

Kabla ya mchezo huo, Argentina ilitawaliwa na skendo ya kupendelewa na waamuzi katika mechi zilizopita, hasa dhidi ya Misri na Uswis.

Kwa nyakati tofauti, mamlaka za soka za mataifa hayo zilipeleka malalamiko yao FIFA zikidai kuwa waamuzi walikuwa upande wa Argentina.

Related articles

Recent articles