27.4 C
New York

Sikia hii kuhusu Fury, Joshua

Published:

LONDON, Uingereza

MWAKA huu haiushi. Huenda Tyson Fury na Muingereza mwenzake wa ngumi za uzito wa juu, Anthony Joshua, wakazichapa kama si Oktoba, basi Novemba, 2026.

Taarifa za zinadai kuwa pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa ndondi duniani litapigwa katika Uwanja wa Wembley jijini London, Uingereza.

Anayesimamia uwezekano wa Fury na Joshua kumaliza ubishi ni promota raia wa Saudi Arabia, Turki Alalshikh, ambaye anataka pambano hilo lipigwe Uingereza.

Awali, zilikuwepo taarifa kuwa Fury na Joshua watafunga safari hadi Marekani litakakofanyika pambano hilo.

Hata hivyo, Juni, 2026, promota wa Joshua, Eddie Hearn, alikanusha alisema pambano halitopelekwa Marekani na badala yake litapigwa Uingereza.

Fury na Joshua, kila mmoja anatarajiwa kuwa na pambano moja kabla ya vita yao ya mwishoni mwa mwaka huu (2026).

Bingwa wa zamani wa WBC, Fury (37), atamvaa Mariusz Wach wa Poland, pambano litakalopigwa Julai 24, 2026, nchini Thailand.

Siku moja baadaye, Joshua (36), atakabiliana na Kristian Prenga na pambano hilo litapigwa katika ardhi ya Saudi Arabia.

Related articles

Recent articles