27.4 C
New York

Pogba afunguliwa mlango Monaco

Published:

MONACO, Ufaransa

MTENDAJI Mkuu wa klabu ya soka ya Monaco, Thiago Scuro, amesema wako tayari kumruhusu kiungo Paul Pogba kuondoka klabuni hapo.

Kwa mujibu wa Scuro, Pogba ataondoka katika klabu ya Ligue 1 kupitia dirisha kubwa la usajili majira haya ya kiangazi.

Scuro amekiri kuwa usajili wa Mfaransa huyo wa mwaka jana klabuni hapo haujazaa matunda.

“Labda ataondoka, labda atabaki. Bado ni ngumu. Tunamuheshimu mno,” amesema bosi huyo.

Klabu zinazompigia hesabu nyota huyo wa zamani wa Manchester United ni pamoja na za Ligi Kuu ya Marekani (MLS) na Saudi Arabia.

Related articles

Recent articles