MIAMI, Marekani
WINGA Riyad Mahrez ametangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya soka ya Taifa ya Algeria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari maarufu wa Italia, Fabrizio Romano, Mahrez amethibitisha hilo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha BeIN Sports.
Hatua ya Mahrez kujiweka pembeni imekuja baada ya Algeria kutandikwa mabao 2-0 na Uswis na kuishia hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia.
Mahrez (35), ameiacha Algeria akiwa ameifungia mabao 40 na kutoa ‘asisti’ 45 katika michezo 119.
Alikuwa kwenye kiwango bora zaidi walipotwaa ubingwa wa fainali za AFCON za mwaka 2019.
Baada ya kuiacha Algeria, sasa nyota huyo wa zamani wa Manchester City ataelekeza nguvu kwenye klabu yake ya Al-Ahli ya Saudi Arabia.


