36.8 C
New York

Mama yake Burna Boy ataka mkwe, wajukuu

Published:

LAGOS, Nigeria

MAMA yake Burna Boy ambaye pia ndiye meneja wake, Bose Ogulu, amemtaka staa huyo wa muziki kuoa na kupata watoto.

Ujumbe huo umekuja baada ya Burna Boy kusherehekea ‘bitrthday’ ya kutimiza umri wa miaka 35 jana, Julai 2, 2026.

Aliyevujisha ujumbe wa ‘bi mkubwa’ ni mtu wa karibu wa Burna Boy, Richie 7, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Snapchat.

Miaka michache iliyopita, Burna Boy alisema hana mke wala mtoto kwa kuwa haitaji familia.

Kwa mujibu wake, ratiba yake ya kazi inambana, hivyo hatokuwa na muda wa kukaa na familia nyumbani

Related articles

Recent articles