37.6 C
New York

Arsenal yatia nanga kwa kipa huyu

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Arsenal iko kwenye hatua nzuri ya kukamilisha usajili wa kipa aliyeondoka Leeds United baada ya kumaliza mkataba wake, Illan Meslier.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anamtolea macho Meslier akiamini anatosha kuziba pengo la Kepa Arrizabalaga anayeweza kuondoka.

Arrizabalaga (31), amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Arsenal lakini Arteta haonekani kumuweka kwenye hesabu zake za msimu ujao.

Meslier ana umri wa miaka 26 na ameondoka Leeds United akiwa amecheza mechi 215, huku 70 akiwa hajaruhusu bao.

Kipa huyo raia wa Ufaransa ana uzoefu wa Ligi Kuu ya England (EPL) kwani alicheza mechi zake 107 akiwa na Leeds United.

Related articles

Recent articles