37.6 C
New York

Kocha Ubelgiji amtaja aliyeiua Senegal

Published:

MIAMI, Marekani

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Ubelgiji, Rudi Garcia, amesema nahodha wake, Youri Tielemans, ndiye mchezaji aliyekuwa na mchango mkubwa katika mechi yao dhidi ya Senegal.

Katika mchezo huo wa hatua ya 32 Bora ya msimu huu wa Kombe la Dunia, Senegal walitandikwa mabao 3-2.

Senegal wanaweza kujilaumu wenyewe kwani walishatangulia kwa mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Habib Diarra na Ismaila Sarr.

Hata hivyo, Ubelgiji walisawazisha kupitia kwa Tielemans aliyetupia mawili, na Romelu Lukaku.

“Tukiwa sare ya mabao 2-2, katika dakika ya 120, bado Youri alikuwa na nguvu. Alifanikiwa sana,” amesema kocha Garcia.

Related articles

Recent articles