ACCRA, Ghana
WATU 12 wameripotiwa kupoteza maisha katika mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini Ghana, ukiwamo Mji Mkuu wa Accra.
Mvua iliyonyesha ni ya kiwango cha milimita 140 mjini Accra, kwa mujibu wa Rais wa Ghana, John Dramani Mahama.
Kiwango hicho cha mvua ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Ghana Kwa miaka ya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa ya kikosi cha uokoaji, mtoto mmoja ni sehemu ya watu 12 waliopoteza maisha, pamoja na wanawake watatu na wanaume nane.
Mamlaka zimeongeza kuwa jumla ya watu 470 wameokoloewa kwa kutolewa kwenye maeneo yaliyozingirwa na mafuriko hayo.


