MIAMI, Marekani
MIROSLAV Koubek wa timu ya soka ya Taifa ya Czech amekuwa kocha wa tatu kupoteza kibarua msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.
Czech iliishia hatua ya makundi ikiwa Kundi A baada ya kukusanya pointi moja pekee katika michezo mitatu.
Ikumbukwe, Czech walikuwa kwenye kundi lenye timu zingine tatu, ambazo ni Korea ya Kusini, Afrika Kusini, na Mexico.
Koubek amepoteza kazi ikiwa ni miezi michache tu tangu alipoajiriwa wakati wa mechi za kufuzu za play-off za Kombe la Dunia.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 74, aliiwezesha Czech kufuzu akizifunga kwa penalti Ireland na Denmark.
Chini yake, timu hiyo ilirejea Kombe la Dunia baada ya miaka 20 ya kukosa ushiriki wa michuano hiyo ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).


