24.8 C
New York

Mfumo wa E-Delivery kutathmini matokeo ya miradi utekelezaji wa Dira 2050

Published:

Na mwanishi wetu, Gazetini

KATIKA utekelezaji wa Dira 2050, Mfumo mpya wa Kitaifa wa kusimamia Mipango na Miradi ya Maendeleo wa e-Delivery wa Tume ya Taifa ya Mipango imeelezwa kuongeza uwazi, uwajibikaji, ufanisi, na usimamizi wa miradi ya maendeleo yenye matokeo makubwa kwa wananchi.

Mfumo huo ambao utaanza Julai Mosi, 2026 sambamba na Dira 2050 katika matumizi yake, hakuna mradi wowote utakaotekelezwa bila kusajiliwa kwenye mfumo huo ambao utausaidia Serikali kufahamu mahitaji halisi ya rasilimali fedha, kupanga na kuainisha vipaumbele vya maendeleo, kutathmini hali ya utekelezaji wa mradi, kufanya ufuatiliaji na tathmini, pamoja na kupokea taarifa za utekelezaji kupitia Mfumo wa huo wa e-Delivery.

Akizungumza Alhamisi, Juni 25, 2026 katika mafunzo yanayoendeshwa na Tume ya Taifa ya Mipango jijini Arusha kuhusu matumizi ya mfumo huo Meneja Mifumo na Kujenga Uwezo kutoka Tume hiyo Wiranga Giraguti amesema e- Delivery unakidhi mahitaji ya sasa na baadaye katika usimamizi wa miradi yote ya maendeleo, kwani unawalazimu watendaji kuibua na kutekeleza miradi ambayo inaendana na malengo ya Dira 2050 kwa kupitia hatua zote muhimu ambazo ni kuibuliwa kwa wazo, uchambuzi wa andiko, uidhinishaji, utekelezaji, ufuatiliaji, hadi tathmini ya mwisho ya matokeo.

Ameeleza kuwa ili kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa ipasavyo katika miradi yote ya Maendeleo mfumo huo wa e-Delivery umeunganishwa na mifumo mingine muhimu ya kitaifa ikiwemo MUSE, CBMS, PlanRep I na II, D-Fund, NaPA, NeST, ERBMIS, na CRBMIS ambapo itasaidia taarifa za kifedha, manunuzi, na bajeti kupatikana kwa urahisi na kwa wakati na kuepuka urudufu wa taarifa.

Zaidi ya Wataalamu 600 wa mipango, sera, ufuatiliaji na tathmini (M&E), pamoja na TEHAMA kutoka wizara, taasisi, mikoa, na halmashauri mbalimbali wameshapatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo huo na Tume ya Taifa ya Mipango na lengo ni kuwafikia watendaji zaidi ya 1,200.

Related articles

Recent articles