19 C
New York

Arsenal, United vita nzito kisa kiungo

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU za Arsenal na Manchester United zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, ambaye ana thamani ya Pauni milioni 60.

Scott (22), ni kiungo wa ulinzi na msimu uliopita alikuwa na umiliki wa mpira mara 195. Pia, alikuwa na wastani wa kucheza mipira ya juu kwa asilimia 56.

Hata hivyo, huenda ikawa rahisi zaidi kwake kupenya kikosi cha kwanza cha Man United kuliko Arsenal yenye Declan Rice, Myles Lewis-Skelly na Martin Zubimendi.

Kwa Man United, nafasi hiyo ya kiungo wa ulinzi ina Kobbie Mainoo na Manuel Ugarte ambaye hata hivyo anahusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford.

Je, kiungo huyo wa kimataifa wa England ataibukia Old Trafford au Emirates?

Related articles

Recent articles