TORONTO, Canada
TIMU ya soka ya Taifa ya Croatia sasa inahitaji ushindi tu mbele ya Ghana ili kufuzu hatua inayofuata (32 Bora) ya msimu huu wa Kombe la Dunia.
Ni baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Panama, ukiwa ni mchezo wa Kundi L, ambao ni wa 200 kwa nahodha Luka Modric tangu alipoanza kuitumikia Croatia.
Modric (40), alicheza kwa dakika 81 na anakuwa mchezaji wanne katika historia ya soka la wanaume kufikisha idadi hiyo ya michezo.
Katika mechi hiyo, dakika 45 za mwanzo zilimalizika kwa suluhu, kabla ya mshambuliaji wa Osasuna, Budimir, kutokea benchi na kufunga bao pekee hilo.
Kwa matokeo hayo, Panama imeyaaga mashindano baada ya kupoteza mechi zote mbili.


