19 C
New York

Deschamps afiwa na mama yake, aondoka Kombe la Dunia

Published:

NEW YORK, Marekani

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amerejea jijini Paris baada ya taarifa za kifo cha mama yake mzazi.

Ni kwa maana hiyo, Deschamps atakosekana kwenye benchi wakati Ufaransa itakapocheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Norway (Juni 26, 2026).

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF), kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 ameruhusiwa kwenda kwenye mazishi.

Ufaransa ikiwa Kundi I, imeshakata tiketi ya kuingia hatua ya 32 Bora baada ya ushindi wa mechi mbili za awali, ikizifunga Senegal na Iraq.

Katika taarifa iliyotolewa na Rais wa FFF, Philippe Diallo, kocha msadizi, Guy Stephan, atashika kwa muda nafasi ya Deschamps.

Related articles

Recent articles