MIAMI, Marekani
KLABU ya Inter Miami ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) imethibitisha kuinasa saini ya kiungo wa kimataifa wa Brazil, Casemiro.
Casemiro amejiunga na timu hiyo ya Lionel Messi akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United akiwa amemaliza mkataba.
Awali, mwandishi wa habari za michezo wa Italia, Fabrizio Romano, alisema Casemiro atajiunga na vigogo hao wa MLS.
“Pande mbili zimefikia makubaliano, kinachosubiriwa ni Mbrazil huyo kusaini na kutambulishwa,” alisema.
Kwa sasa Casemiro yuko kwenye fainali za Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Brazil.


