21.2 C
New York

Mganga ‘aliyemkomesha’ Ronaldo ahamia kwa Harry Kane

Published:

ACCRA, Ghana

MGANGA wa kienyeji raia wa Ghana ambaye alidai kumsababishia majeraha Cristiano Ronaldo wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, ameibuka na kusema sasa amehamia kwa Harry Kane.

Nana Kwaku Bonsam ameibuka zikiwa zimebaki saa chache kuelekea mchezo wa kesho Juni 23, 2026 kati ya England na Ghana.

Kwa mujibu wa mganga huyo, yuko kazini kuhakikisha straika wa England, Kane, hatofanya chochote kwa muda wote wa mchezo huo.

Wakati wa fainali za mwaka 2014, Bonsam alidai kuwa ndiye aliyemfanyia ‘mavituz’ Ronaldo na kusababisha staa huyo kuumia goti.

Kane ni moto wa kuotea mbali msimu huu wa Kombe la Dunia, ambapo tayari ana mabao mawili katika michezo miwili aliyocheza.

“Namfungia kazi Harry Kane. Nimeshaonesha uwezo wangu hapo awali (kwa Ronaldo), kwa hiyo najua cha kufanya,” amesema Bonsam akihojiwa na Gazeti la Daily Star.

Related articles

Recent articles